TIBA NA MAGONJWA YA MACHO Written By Elphas Mkumbo on Tuesday, 19 September 2017 | 23:01 karibu katika mfululizo wa makala za afyaya macho, kama ulipitwa na somo lililotangulia basi bonyeza HAPA kuweza kusoma tena. . Leo tutazungumzia tatizo la wekundu wa macho au kitaalamu conjunctivitis. CONJUNCTIVITIS NI NINI?? Macho mekundu au conjunctivits kwa kitaalam ni maradhi yanayohusisha ukuta wa nje wa sehemu ya mbele ya jicho ijulikanayo kama conjunctiva. Conjuctiva ni ukuta ambao hulinda sehemu nyeupe ya jicho pamoja na ukuta wa ndani wa ngozi ifunikayo jicho, yaani kope. Maradhi haya hutokea baada ya kuvimba kwa ukuta na mishipa midogo ya damu iliyo kwenye ukuta huu. Kuna mambo mengi yanayosababisha macho yawe mekundu. Sababu hizi ni pamoja na maambukizi ya virusi au vimelea vya maradhi aina ya bakteria (mfano bakteria wanaosababisha kisonono). Kemikali zinazosababisha mzio kwa mfano sabuni, mafuta ya kupaka, vumbi au moshi. Inaelezwa, moshi ni sababu ...
Comments
Post a Comment