TIBA NA MAGONJWA YA MACHO

Written By Elphas Mkumbo on Tuesday, 19 September 2017 | 23:01

karibu katika mfululizo wa makala za afyaya macho, kama ulipitwa na somo lililotangulia basi bonyeza HAPA kuweza kusoma tena.. Leo tutazungumzia tatizo la wekundu wa macho au kitaalamu conjunctivitis.

CONJUNCTIVITIS NI NINI??
Macho mekundu au conjunctivits kwa kitaalam ni maradhi yanayohusisha ukuta wa nje wa sehemu ya mbele ya jicho ijulikanayo kama conjunctiva. Conjuctiva ni ukuta ambao hulinda sehemu nyeupe ya jicho pamoja na ukuta wa ndani wa ngozi ifunikayo jicho, yaani kope. Maradhi haya hutokea baada ya kuvimba kwa ukuta na mishipa midogo ya damu iliyo kwenye ukuta huu.

Kuna mambo mengi yanayosababisha macho yawe mekundu. Sababu hizi ni pamoja na maambukizi ya virusi au vimelea vya maradhi aina ya bakteria (mfano bakteria wanaosababisha kisonono).
Kemikali zinazosababisha mzio kwa mfano sabuni, mafuta ya kupaka, vumbi au moshi. Inaelezwa, moshi ni sababu kubwa kwa wazee wanaoishi vijijini.
Maradhi haya hutokea pale vyanzo hivi vinapotoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Maradhi haya husambaa kwa urahisi bila haja ya kugusana bali hata kwa njia ya hewa.
Maradhi haya hushambulia watu wa umri wote ingawa wazee na watoto wachanga hudhurika zaidi kutokana na maradhi haya. Mgonjwa hasa mtoto mchanga anapopata maradhi haya ni vyema kwa mzazi au mlezi kuhakikisha anampeleka kwenye kituo cha afya kwa ajili ya matibabu.

Maradhi haya kwa wengi yanayohitaji huduma ya dharura lakini ni vyema kuhakikisha kuwa mtaalam wa afya anachunguza ili kufahamu chanzo kabla ya matibabu.

DALILI KUU.
  • Maradhi haya huwa na dalili na miongoni mwake ni sehemu nyeupe ya jicho yaani sclera na ngozi ya ndani ya kope kubadilika rangi na kuwa nyekundu, macho kuwasha na kutoa machozi.


  • Baadhi ya wagonjwa huhisi kama vile macho yanaungua na baadhi hushindwa kuona vizuri, hii hutokana na kuvimba kwa sehemu ya ukuta wa mbele wa jicho yaani conjunctiva.
  • Macho kutoa machozi mengi kila mara,
  • Kuhisi kama kuna kitu kama mchanga kwenye macho.
  • Dalili nyingine ni macho kutoa matongotongo kwa wingi hasa mgonjwa akiwa amelala kiasi cha kushindwa kuyafungua kutokana na wingi wake. Wapo wanaoshindwa kuona vizuri kwenye mwanga mkali.

Inashauriwa kumuona daktari wakati wowote moja ya dalili hizi zinapojitokeza au unapohisi jicho au macho yako hayako sawa ili kubaini tatizo na kulitibu kwa muda muafaka kabla athari zake hazijawa kubwa.

Mara baada ya kuona dalili hizi za maradhi, inashauriwa kumuona mtaalamu wa afya ambaye atasikiliza historia ya maradhi na kufanya vipimo ambavyo vitasaidia kugundua chanzo na kushauri matibabu yanayofaa.

Matibabu
 1.BACTERIA; Matibabu ya macho mekundu hutegemea chanzo. Kama chanzo cha maradhi ni bakteria basi daktari hupendekeza antibaiotiki (antibiotics). Dawa hizi huwa kwenye mfumo wa matone au za kupaka kwenye macho. Kutegemea na ukubwa wa maradhi daktari pia huweza kutoa vidonge. Dawa za kupaka huhitajika kupakwa ndani ya ukuta unaofunika macho (eyelid) mara mbili ama 3 kwa siku kwa siku mpaka saba. Kadri mgonjwa navotumia dawa basi huedelea kupata nafuu, inashauriwa kumeza antibiotics kama ulivoelekezwa na Dactari wako.



2.    2VIRUSI:  aina nyingine ya wekundu wa macho ambayo mara nyingi husababishwa na virusi wanaoeneza mafua, na aina hii kikawaida huisha baada ya siku 4 mpaka 7. Kama macho mekundu yamesababishwa na virusi, kwa bahati mbaya, huwa hakuna dawa ya kuyatibu. Habari njema ni kuwa kama ilivyo kwa maradhi ya mafua, mara nyingi maradhi ambayo husababishwa na virusi huisha yenyewe baada ya siku chache kwani kinga ya mwili huwa na uwezo wa kuua virusi hivi na hivyo mgonjwa kupona. Hakikisha unachukua tahadhari ili kuepusha kusambaa kwa ugonjwa kwenda kwa mtu mwingine kwa kuosha mikono mara kwa mara na kuepuka kushikana mkino na watu wazima. Kama tatizo likizidi Zaidi basi muone Dactari upate ushauri na tiba Zaidi.

3    3.  KEMIKALI: Endapo chanzo cha macho mekundu ni kemikali basi daktari atashauri mgonjwa aoshe macho na maji safi na kuhakikisha jicho au macho yanakuwa safi muda wote kwa kuyasafisha mara kwa mara mpaka atakapopata nafuu au kupona kabisa.

4.  4.ALEJI (MZIO) Wagonjwa  wanaougua kutokana na mzio. Kwa chanzo hiki, atatoa dawa za kupunguza madhara ya mzio ili kukabiliana maradhi husika.

                      KINGA
       Kama yalivyo magonjwa mengi, zipo namna za kuepuka macho mekundu.
1  .      Inashauriwa kuepuka kufikicha macho mara kwa mara kwani hii ni namna inayosambaa kirahisi zaidi         ugonjwa huu.
2  .       Macho mekundu yanayosababishwa na virusi husambaa kwa haraka na kwa njia nyepesi zaidi. Kwa maana hii, ni vyema kwa wagonjwa kuhakikisha hawashikani mikono wala hawatumii vifaa vya kujiremba vinavyotumiwa na watu wengine.
3  .       Kwa wagonjwa, inashauriwa kuhakikisha wananawa mikono kwa maji safi muda wote ili kuzuia uwezekano wa kuwaambukiza watu walionao karibu.
4   .       Safisha macho yako kwa maji safi na salama mara kwa mara. Hii husaidia kuondoa vyanzo vya maradhi au kupona upesi kama umeshaambukizwa. Ni vyema kuhakikisha unaosha mikono mara zote unapomaliza kusafisha macho.
5   .       Kama unatumia vifaa vya urembo basi hakikisha mtu mwingine yoyote hatumii vifaa hivyo kwa wakati huo ili kuzuia kusambaa kwa maradhi hayo.
6   .       Kama unaweza kuvaa miwani maalum ya kuzuia mwanga mkali wa jua (wengi tunaita miwani ya jua) basi unashauriwa kuitumia ili kupunguza macho yasiumie zaidi.
7   .       Inashauriwa, usihamishe dawa ya macho kutoka kwenye jicho lenye maradhi na kuipeleka kwenye jicho salama kwani unaweza kuliambukiza wala kufikicha jicho lenye maambukizi halafu lisiloathirika.
8  .       Mwisho Kwa wanafunzi, uongozi wa shule unatakiwa kumshauri mtoto kukaa nyumbani mpaka atakapopona ili kuepuka uwezekano wa kuwaambukiza wengine.

Madhara ya tatizo hili.
Mara nyingi maradhi haya hayana madhara makubwa. Wagonjwa wengi hupona kabisa isipokuwa wachache ambao hupata makovu yanayobaki kwenye conjunctiva. Makovu haya husababisha changamoto ya kuona vizuri.

Kwa watoto wadogo ni vyema kuwapeleka hospitali mara tu mzazi au mlezi anapoona moja ya dalili zilizotajwa.. 

wasiliana nasi kwa namba 0762336530 email  elifasimkumbo@gmail.com. kupata maelekezo ya jin si ya kufika ofsini kwetu hapa Dar maeneo ya Karume Chinga Complex kwa ushauri na kupata virutubisho na dawa kwa ajili ya matatizo ya macho.

Comments

  1. Je mm macho yangu hayaumi pia ya naona vizuri, lkn ni mekundu ,je yanga tatizo gani

    ReplyDelete
  2. Mimi macho yangu yana uma n'a kutoa machozi n'a kuwashaLakini si mekundu je ! Matatizo ?

    ReplyDelete
  3. Mm mwanangu anasumbuliwa na macho ya kuwasha,kuvimba,nakutoa machozi atumie dawa gani ikiwa niko mbali na hispitali naomba msaada wa tiba au ushauli wa mawazo

    ReplyDelete
  4. Mimi macho yangu yanatoa matongotongo kama vikamba na ukichezea jicho sana yanaingia ukungu,sijui chanzo ni nini?

    ReplyDelete
  5. Vipi kuhusu mtu kutokwa na matongotongo mara kwa mara hii husababishwa na nini

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog