Posts

Showing posts from December, 2017
Image
Image
Ugonjwa wa figo na sababu za kushindwa kufanya kazi Assalam aleykum wasikilizaji wapenzi na karibuni katika kipindi kingine cha Ijue Afya Yako. Kipindi ambacho hujadili na kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu afya na tiba yakiwemo magonjwa na namna ya kujikinga nayo ili kuiwezesha jamii kuimarisha afya kwa ujumla. Katika kipindi chetu cha leo na vinavyofuata tutazungumzia matatizo ya figo na kile kinachosababisha viungo hivyo muhimu mwilini vishindwe kufanya kazi. Tumeamua kuzungumzia maudhui hiyo kutokana na watu wengi katika jamii yetu kukabiliwa na matatizo tofauti ya figo ambayo matibabu yake ni yenye gharama kubwa na ambayo pia husababisha baadhi kupoteza maisha. Hapa duniani kuna maradhi ya aina nyingi yanayotisha, kusumbua binadamu, kuwatia ulemavu na hata kuwa chanzo cha uchumi kutetereka na wakati mwingine kusababisha vifo. Miongoni mwa maradhi hayo ni kuharibika kwa figo au kushindwa kufanya kazi. Ugonjwa huo si tu kwamba huleta maumivu kwa mgonjwa, bali...
Image
atibabu ya ugonjwa wa figo ukubwa wa hati       Kichapishi  Comments (2) Ni matumaini yangu kuwa hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni katika kipindi chenu hiki cha Ijue Afya Yako. Wiki iliyopita tulieleza kwa urefu kuhusu ugonjwa wa figo na kufafanua jinsi mtu anavyoweza kuugua ugojwa huo. Wiki hii pamoja na mambo mengine tutaeleza jinsi ugonjwa huo unavyoweza kutibika. Basi msiondoke kando ya redio zenu ili muweze kufahamu namna ya kutibu ugonjwa huo. Tulisema kwamba dalili ya kwanza ya kuugua ugonjwa wa figo ni kupungua kwa kiasi cha mkojo. Dalili nyingine ni maji kujaa mwilini, madini za mwili kuwa juu hasa ya potasiamu, asidi nyingi, na mgonjwa kujisikia au kuwa na matatizo katika moyo na anaweza pia kuwa na matatizo katika ubongo. Mgonjwa pia anaweza kukosa hamu ya kula chakula chochote na hali hiyo kumfanya au kusababisha adhoofike mwili. Nyongeza za dalili za mtu kuugua ugonjwa wa figo hasa kwa wale wagonjwa ambao hawagunduliki mapem...
Image
Ugonjwa sugu wa figo (Chronic Kidney Disease) Ni matumaini yangu kuwa hamjambo wapenzi wasikiliza, na katika kipindi chetu cha leo tunaendelea kujadili magonjwa ya figo na leo tutazungumzia ugonjwa sugu wa figo au chronic kidney disease kwa kimombo. Ugonjwa huu hutokea pale figo zinapopoteza uwezo wa kutenda kazi ambayo hutokea taratibu, na huchukua muda wa takribani miezi kadhaa hata miaka. Figo zinapopoteza uwezo wake wa kutenda kazi, kusanyiko na limbikizo la maji, uchafu na sumu hutokea mwilini mwa mgonjwa na pia husababisha kutokea kwa maradhi mengine kama tulivyoyataja katika vipindi vilivyopita. Lakini huenda ukajiuliza swali kwamba je, kuna tofauti gani kati ya ugonjwa sugu wa figo na kushindwa figo kufanya kazi kwa ghafla yaani Acute Renal Failure? Tofauti ni kwamba ARF hutokea ghafla, huchukua muda mfupi kati ya siku hadi wiki kadhaa kuwa tatizo kubwa zaidi. Tofauti nyingine ni kuwa kushindwa kufanya kazi figo kwa ghafla hutokana na tatizo linaloathiri figo mo...
Image
Homa ya Mapafu Kwa watoto (Pneumonia) Ni wakati mwingine umewadia wapenzi wasikilizaji wa kutegea sikio kipindi cha Ijue Afya Yako. Wiki hii tunaendelea kuzungumzia magonjwa ya watoto wadogo na leo tutajadili ugonjwa wa homa ya mapafu kwa watoto maarufu kma Pneumonia. Ili kuyajua maradhi hayo yanayosabisha vifo vya watoto wengi duniani kote, ungana nami hadi mwisho wa kipindi hiki. Homa ya mapafu ni aina ya maambukizi yanayoathiri mapafu. Ni ugonjwa ambao unaua watoto wengi hasa katika nchi zinazoendelea duniani. Inakadiriwa kwamba watoto karibu milioni 1.6 walio chini ya miaka 5 maisha yao hupotea kila mwaka kutokana na ugonjwa huu. Kutokana na vifo vingi vinavyotokana na homa ya mapafu tarehe 12 ya mwezi wa Novemba kila mwaka imefanywa kuwa siku rasmi ya homa ya mapafu duniani, ili kuwajuza walimwengu maradhi hayo na kuwahamasisha namna ya kujikinga na kuyatibu. Kabla hatujaendelea mbele ni bora kwanza tuwaeleze wasikilizaji wetu muundo wa mapafu ulivyo na sehemu am...
Image
Tatizo la mzio au allergy Ni matumaini yangu kuwa hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni katika kipindi kingine cha Ijue Afya Yako. Leo tutatungumzia tatizo la mzio au alegi. Ili kufahamu tatizo hilo na kujua jinsi ya kukabiliana nalo ungana nami hadi mwisho wa kipindi hiki. Mzio au aleji (allergy) ni matokeo ya mpambano uliopitiliza kati ya kinga ya mwili na kitu chochote ambacho kwa ujumla huwa hakina madhara kwa mwili pale inapotokea kimeingia ndani ya mwili au kimegusa sehemu fulani ya mwili. Mpambano huu ndio husababisha mtu kuwa na dalili za aleji au mzio. Kwa kawaida kinga ya mwili huulinda mwili dhidi ya vitu mbalimbali hatari kwa afya kama vile vimelea vya magonjwa kama bakteria na virusi, lakini wakati mwingine inaweza kupambana pia na vitu ambavyo havina madhara yeyote kwa mwili ambavyo huitwa allergens. Baadhi ya vitu vinavyosababisha mzio ni pamoja na vumbi, baadhi ya dawa, baadhi ya vyakula, kung'atwa na wadudu kama vile nyuki, aina fulani ya u...
Image
Aleji au mzio unaosababishwa na dawa Ni matumaini yangu kuwa hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni katika kipindi kingine cha Ijue Afya yako. Wiki iliyopita tulianza kuzungumzia tatizo la aleji au mzio, mada ambayo leo pia tutaendelea kuijadili. Pia tutazungumzia aleji inayosababishwa na dawa na namna ya kujikinga nayo. Tafadhalini jiungeni nami hadi mwisho wa kipindi. &&&&&& Kama tulivyosema wapenzi wasikilizaji mzio au aleji ni matokeo ya mpambano uliopitiliza kati ya kinga ya mwili na kitu chochote ambacho kwa ujumla huwa hakina madhara kwa mwili, inapotokea kimeingia ndani ya mwili au kimegusa sehemu fulani ya mwili. Unachopaswa kukijua kuhusu mzio ni hali inayotokea wakati seli za mwili wako zinapokataa kitu ambacho kwa mtu wa kawaida hakina madhara. Mzio hujitokeza kwa alama au dalili mbalimbali na huleta matokeo yenye ishara nyingi mwilini. Kuna aina mbili kuu za mizio, zile zinazosababishwa na kitu ambacho kiko nje ya mwili na hu...
Image
Afya Maambukizo katika njia ya Mkojo (UTI) ukubwa wa hati       Kichapishi  Comments (6) Ni matumaini yangu kuwa hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni katika kipindi chenu chenye faida tele cha Ijue Afya Yako. Leo tutazungumzia tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo Urinary Tract Infection ugonjwa ambao unawasumbua sana wanawake wengi na watoto katika nchi nyingi zinzoendelea. &&&&&& Maambukizi katika njia ya mkojo au kama unavyojulikana kwa wengi UTI huathiri mfumo wa mkojo ikiwa ni pamoja na ureter ambayo ni kama bomba linalosafirisha mkojo kutoka kwenye figo, pia kibofu cha mkojo na urethra. Ugonjwa huu unaathiri zaidi kibofu cha mkojo na urethra lakini unaweza pia kuathiri figo. Maambukizi haya yakiathiri sehemu za chini za kibofu cha mkojo kitaalamu huitwa simple cystitis au Bladder infection, na maambukizi hayo yakitokea sehemu za juu za mfumo wa mkojo huitwa pylonephritis au kidney infection. Ugonjwa hu...
Image
Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, mwili wako unahitaji virutubishi ili kusaidia ukuaji wa mwili, kama ni kijana mwili wako una mahitaji maalumu unayoyahitajia kudhamini makuzi ya kiafya ya mwili wako wakati wa utu uzima na wakati unapokuwa mtu mzima unahitaji kuwa na uzito uliolingana na mwili wa wastani. Tukiangalia katika upande wa Akina mama wajawazito na wale wanaonyonyesha nao pia wana vyakula vyao maalumu wanavyohitajia tofauti kabisa na wanawake wengine. Uchunguzi wa kitiba uliofanywa unaonyesha kuwa, hali ya kiafya ya mama mjazito huwa na athari mbalimbali kwa mtoto atakayezaliwa. Vile vile kuna ushahidi mkubwa kuwa magonjwa sugu ya watu wazima huanzia wakati mtoto bado akiwa tumboni mwa mama yake akiwa katika hali ya kiluilui au (foetus). Kwa hivyo akina mama wajawazito wanashauriwa kuzingatia vyakula wanavyokula kabl...
Image
Saratani ya Ngozi (Melanoma)     Ahlan wa Sahlan wapenzi wasikilizaji na karibuni katika kipindi kingine cha Ijuwe Afya Yako. Kama mnakumbuka wiki iliyopita tulianza kujadili magonjwa yanayoshambulia ngozi ambapo tulizungumzia juu ya ugonjwa wa mba na pia matibabu yake. Wiki hii katika muendelezo wa kuzungumzia magonjwa yanayoathiri ngozi tutajadili ugonjwa wa saratani ya ngozi. &&&&&&&&&& Kansa ya Ngozi Ni Tatizo Kubwa Leo Jarida la The Merck Manual limeeleza kwamba kansa ya ngozi ndiyo kansa inayopata watu wengi zaidi ulimwenguni. Nchini Marekani, mtu mmoja kati ya kila watu 6 hadi 7 hupatwa na aina fulani ya kansa ya ngozi. Lakini idadi ya watu wanaopatwa na kansa hiyo inaongezeka. Katika kitabu The Skin Cancer Answer, Dakta I William Lane anasema: "Sasa inakadiriwa kwamba asilimia 50 ya watu ambao hufikisha umri wa miaka 65 hupatwa na aina fulani ya kansa ya ngozi." Kulingana na Taasisi ya Magonjwa ya Ngozi...